7 – Mungu Msaada Wetu

( 103 – O God, Our Help )

  1. Mungu Msaada wetu tangu miaka yote,Ndiwe tumaini letu la zamani zote.
  1. Kivuli cha kiti chako ndiyo ngome yetu,Watosha mkono wako ni ulinzi wetu.
  1. Kwanza havijakuwako nchi na milima,Ndiwe Mungu; chini yako twakaa salama.
  1. Na miaka elfu ni kama siku moja kwako,Utatulinda daima. tu wenyeji wako.
  1. Bwana msaada wetu tangu miaka yote,Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.
WhatsApp