64 – Piga Panda

( 368 – Watchman, Blow the Gospel Trumpet )

1. Piga panda ya Injili, onyesha watu wote;
Ili anaye sikia Atubu aokoke.

Piga panda ya Injili, uipige kwa nguvu;
Mungu amekuagiza mateka wawe huru.

2. Uipige vilimani, kwa kila tambarare;
Pande zote, miji yote isikie Injili.

3. Uipige mipakani, barabarani pia;
Iwatangazie wote, wanakwitwa na Baba.

4. Uipige! Watu wengi wataka wawe huru;
Waanbie kwamba Yesu asema “Njoni Kwangu.”

WhatsApp