63 – Niuonapo Msalaba

( 154 – When I Survey the Wondrous Cross )

1. Niuonapo Msalaba,
Kristo aliponifia;
Kwangu pato ni hasara.
Kiburi nakichukia.

2. Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa sadaka yako;
Upuzi sitake tena,
Zi chini ya damu yako.

3. Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwangwa pendo na hamu.
Ndako pweke hamu hiyo.
Pendo zako zimetimu

4. Vitu vyote vya dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia,
Nafsi, mali na maisha.

WhatsApp