61 – Bwana, Nami

( 456 – My Lord and I )

1. Nimemwona rafiki Wa thamani kubwa,
Ana ni penda kwa ‘pole, Kwa pendo amini:
Kuishi kutengwa naye, La, huku siwezi,
Tunakaa pamoja: Bwana nami.

2. Pengine ninachoka, Mimi mdhaifu,
Ndipo ninamtehemea, Alivyoalika;
Huniongoza njiani Pahali pa nuru
Twatembea pamoja Bwana nami.

3. Namweleza huzuni Nafuraha yangu,
Vile vinavyosumbua Vinavyopendeza;
Huniagiza kutenda Yanayonipasa
Twazungumza pamoja Bwana nami.

4. Ajua natamani Kuwavuta watu,
Hivyo ananipeleka Kutangaza neno;
Nitangaze pendo lake, Kwa nini akafa;
Twahubiri pamoja Bwana nami.

WhatsApp