59 – Fanyeni Kazi Zenu

( 375 – Work, for the Night Is Coming )

  1. Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;
    Kesheni saa zenu vumilieni:
    Kwa Yesu tumikeni na hiyo Injili.
    Sana wahubirini watu wa mbali.
  1. Fanyeni kazi zenu giza yasongea;
    Na wengi wenzi wenu wamo gizani.
    Msipoteze moja dakika ni hizi;
    Mwana atarejea mwisho wa kazi.
  1. Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;
    Wote walio kwenu apenda Mungu:
    Na sisi tumjuaye na tuwafundishe,
    Ili Yesu ajaye tumfurahishe.
WhatsApp