57 – Usikatae Kazi

( Asked Not To Be Excused )

  1. Usikatae Kazi yake Bwana; Ukae tayari Kuifanya kazi;
    Uende po pote Mungu akwitapo, Nawe utaona Furaha kazini.

Njoo, We! Usiikatae; Njoo, We! Uifanye kazi;
Usiikatae Kazi yake Bwana, Ili hatimaye usikatazwe juu.

  1. Usiikatae Kazi yake Bwana; Kwa nini kawia? Fanya kazi leo.
    Mavuno meupe, Wachache Wavuni, Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana.
  1. Usiikatae Kazi yake Bwana, Kukataa pendo Kwako ni Hatari.
    Saa ya rehema, Yesu akiomba, Ziungame dhambi, Zifutwe mbinguni.
WhatsApp