55 – Twapanda Mapema

( 369 – Bringing in the Sheaves )

  1. Twapanda mapema, na mchana kutwa
    Mbegu za fadhili hata jioni,
    Twangojea sasa siku za kuvuna;
    Tutashangilia wenye mavuno.

Wenye mavuno, wenye mavuno,
Tutashangilia wenye mavuno.
Wenye mavuno, wenye mavuno,
Tutashangilia wenye mavuno.

  1. Twapanda mwangani na kwenye kivuli;
    Tushindwe na baridi na pepo;
    Punde itakwisha kazi yetu hapa:
    Tutashangilia wenye mavuno.
  1. Twapanda kwa Bwana mbegu kila siku.
    Tujapoona taabu na huzuni;
    Tuishapo shinda atatupokea:
    Tutashangilia wenye mavuno.
WhatsApp