54 – Nataka Nimjue Yesu!

( 245 – More About Jesus )

  1. Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
    Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

  1. Nataka nimjue Yesu, na nizidi kusikia
    Anenapo kitabuni, kunidhihirisha kwangu.
  1. Nataka tena zaidi, daima kupambanua
    Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.
  1. Nataka nikae, kwa mazungumzo matamu.
    Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake!
WhatsApp