41 – Roho Mtakatifu

( Holy Spirit, Faithful Guide )

1. Roho Mtakatifu, Kiongozi amini;
Utushike mkono Tulio wasafiri;
Utupe kusikia Sauti ya upole;
“Msafiri fuata, Naongoza nyumbani.”

2. Wewe ndiwe rafiki, Msaada karibu;
Tusiache shakani; na tukiwa gizani
Utupe kasikia Sauti ya upole;
“Msafiri, fuata, Naongoza nyumbani.”

3. Siku zetu za kazi, Zikiwa zimekwisha,
Wala hatuna tamaa Ila mbingu na sala;
Utupe kusikia Sauti ya upole;
“Msafiri fuata, Naongoza nyumbani.

WhatsApp