4 – Jina la Yesu, Salamu

( 229 – All Hail the Power of Jesus' Name )

  1. Jina la Yesu, salamu! Lisujudieni,
    Ninyi mbinguni hukumu, Na enzi mpeni.
    Ninyi mbinguni hukumu, Na enzi mpeni.
  1. Enzi na apewe kenu, watetea dini;
    Mkuzeni bwana wenu, Na enzi mpeni.
    Mkuzeni bwana wenu, Na enzi mpeni.
  1. Enyi mbegu ya rehema nanyi msifuni;
    Mmeponya kwa neema, Na enzi mpeni.
    Mmeponya kwa neema, Na enzi mpeni.
  1. Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani.
    Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
    Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
  1. Kila mtu duniani msujudieni,
    Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
    Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
  1. Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.
    Milele sifa ni moja, ni ‘enzi mpeni’.
    Milele sifa ni moja, ni ‘enzi mpeni.’
WhatsApp