36 – Siku Kuu

( O Happy Day )


1. Ni siku kuu siku ile ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele kunyamaza hauwezi.

Siku kuu! Siku kuu! Ya kwushwa dhambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu, ananiongoza miguu.
Siku kuu! Siku kuu! Ya kwoshwa dhambi zangu kuu!

2. Tumekwisha kupatana, mimi bwake, yeye mbwangu,
Na sasa nitamwandama, nikiri neno la Mungu.

3. Moyo tulia kwa Bwana, kiimi cha raha yako;
Huna njia mbili tena: uwe naye, yote ndako.

WhatsApp