26a – Tupe Amani

( 084 – God the Omnipotent )

1.Mungu mtukufu Aliyeumba pepo kuvuma Na radi kali;
Toa neema unapotawala, Tupe amani Bwana wa wema.

2.Mungu wa neema, Nchi imeacha Amri tukufu Na Neno lako;
Hasira zako Zisituharibu, Tupe amani, Bwana wa wema.

3.Mwumbaji wa haki, Watu wabaya Wamedharau Utukufu wako;
Lakini wema wako Utadumu; Endesha kweli Bwana wa wema.

4.Tunakutolea Ibada safi Kwa ajili ya Wokovu wako;
Hivi tunaziimba Sifa zako; Wako uwezo Na utukufu.

WhatsApp