25 – Taji Mvikeni

( 223 – Crown Him With Many Crowns )

1. Taji mvikeni. Taji nyingi sana,
Kondoo mwake Kitini, Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu Alikufa kwangu,
Ni Mfalme mtukufu, Seyidi wa mbingu.

2. Taji mvikeni Mwana wa Bikira;
Anazovaa kichani Aliteka nyara;
Shilo wa manabii Mchunga wa watu
Shina na tanzu ya Yesu wa Bethliehemu.

3. Taji mvikeni Bwana wa Mapenzi;
Jeraha zake ni shani Ni vito nya enzi,
Mbingu haina Hata malaika
Awezae kuziona pasipo kushangaa!

4.Taji mvikeni Bwana wa Salama;
Kote – kote duniani Vita vitakoma;
Nayo enzi yake itaendelea,
Chini ya miguu yake, Maua humea.

WhatsApp