191 – Mkate Wa Mbingu

( 271 – Break Thou the Bread of Life )

1. Mkate wa mbingu mega kwetu;
Ulivyotoa kwa thenashara.
Katika kitabu, twakuona.
Moyo unatweta kukutana.

2. Neno la ukweli libariki;
Tusikie mwito wa upole.
Vizuizi vyote vitakoma.
Tena tutapata uungwana.

3. Uzima na nguvu, utanena;
Nakimbiliza tu kufuata.
Lakini mnyonge ndiye mimi;
Naye Mshindaji ndiye wewe!

WhatsApp