186 – Hatutaagana Tena

( We'll Never Say Good-by )

1. Tuonanapo na rafiki sote twafurahi,
Ila tumepaswa mwishowe kuagana tena.

Hatutaagana tena nyumbani mbinguni,
Kwenye nchi tamu juu, Hatutaagana.

2. Twatumaini kwa furaha tutaonana juu
Na rafiki tulioaga tuishapo shinda.

3. Kule hatutatamka kamwe neno la kuaga,
Tutaimba daima tena nyimbo za furaha.

WhatsApp