185 – Mungu, Mapenzi Makamilifu

( 656 – O Perfect Love )

1. Mungu u mapenzi mtakatifu Yapitayo fahamu za watu
Twanyenyekea sisi wapungufu, Wape baraka wapenzi wetu.

2. Ewe Mapenzi yasiyopimika Twawaombea kitini Mwako,
Wape mapenzi yasiyotindika, Waliooana mbele yako.

3. Ewe uhai, wewe u dhamana Ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana Wasiche maumivu mwishoni.

4. Wape furaha hiyo iwezayo kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itakwayo Katika matata duniani.

5. Waende mbele kusaidiana Maisha yao ulimwenguni;
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, Wafurahi milele mbinguni.

 

 

WhatsApp