18 – Mwokozi, Kama Mchunga

( 545 – Savior, Like a Shepherd )

1. Mwokozi kama mchunga
Utuongoze leo;
Ututume malishoni;
Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako
Umetuvuta kwako.

2. Tu wako, uwe rafiki,
Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde,
Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu tusikie,
Tukiomba, samehe.

3. Umetuahidi kwamba
Utakubali watu,
Utawahurumia na
Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda
Kuwa, mapema.

WhatsApp