16 – Ninakuhitaji

( Blessed Lord, How Much I Need Thee )

1. Bwana ninakuhitaji! Ni mpofu, maskini;
Unishike mkononi, Kwako napata nguvu.

Kila saa, Kila saa Bwana ninakuhitaji;
Kila saa, Kila saa, Unilinde kila saa.

2. Univute na mavazi Ya usikivu wako;
Nguo zangu ni machafu, Nazitamani zako.

3. Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama;
Nenda nani siku zote, U nuru na uzima.

4. Na ikiwa m-beleni Sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha, Unilinde kila saa.

WhatsApp