15 – Nena Mungu

( Speak To My Soul )

1. Nena rohoni yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, “Huachwi upweke.”
‘Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.

Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong’oneza kwa pole wa pendo:
“Daima utashinda, Uhuru niwako.”
Nisikie maneno: “Huachwi upweke.”

2. Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.

3. Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mpanzi yako tena, Daima ‘kusifu.

 

WhatsApp