13 – Yesu Uje Kwetu

( Jesus Thou Hast Promised )

1. Umetuahidi ya kwamba wawili Watatu, kwa jina lako wakija,
Utawabariki kwa hivi leo Twapiga magoti nyumbani pako.

Yesu uje kwetu Utubariki,
Yesu uje kwetu Uwe karibu.

2. Umekuwa nasi siku nyingine Tunakuhitaji mpaka mwisho.
Uje Mkombozi; tupe neema; ‘Tusikie yesu utubariki.

3. Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uzingize.
Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.

WhatsApp