10 – Kristo Wa Neema Yote

( 334 – Come, Thou Fount of Every Blessing )

  1. Kristo wa neema yote imbisha moyo wangu
    Mifulizo yabaraka inaamsha shangwe kuu.
    Unifunze nikupende, nikuandame kote,
    Moyo wangu ukajae furaha natumai.
  1. Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.
    Salama aniongoza hata kule nyumbani.
    Yesu alinitafuta njiani mbali kwake,
    Akatoa damu yake nipone hatarini.
  1. Kweli mimi mwiwa mkubwa wa neema daima;
    Wema wako unifunge zaidi kwako Bwana,
    Ili nisivutwe tena kukuacha ee Mponya,
    Nitwalie moyo wangu uwe wako kamili
WhatsApp