19 – Msalabani Pa Mwokozi

( Down At The Cross )

1. Msalabani pa Mwokozi Hapo niliomba upozi,
Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe.

Na asifiwe, na asifiwe.
Alitukomboa kwa damu, Na asifiwe.

2. Chini ya mti msumbufu Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe.

3. Kwa ajabu ninaokoka, Yesu anakaa moyoni;
Mtini alinifilia, Na asifiwe.

4. Damu ya Yesu ya thamani Huniokoa makosani;
Huniendesha wokovuni, Na asifiwe.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

    [instagram-feed user="mbarikiwamedia"]

Twitter

Recent Comments