60 – Nitakwenda Utakaponituma

( 573 – I'll Go Where You Want Me to Go )

1. Pengine sio milimani Utakaponiita;
Pengine siyo baharini wala palipo vita;
Lakini, nitajibu, na njia siijui.
Bwana, nitajibu, ni tayari Kwenda uniagizapo.

Ukiwa pamoja nami, Bwana, Mlimani, baharini,
Niende utakaponiita; Na fuata uendeko.

2. Pengine leo kuna neno, Neno tamu la pendo,
Ambalo Yesu anataka Ninene kwa upole;
Ukiwa pamoja nami, Bwana, Nitamtafuta leo
Yule aliyepotea mbali: Nitasema upendavyo.

3. Pahali pako bila shaka Pa kuvuna shambani,
Kazi niwezayo kufanya Kwa Yesu Mkombozi;
Hivi nikikutegemea, Kwa kuwa wanipenda,
Mapenzi yako nitafanya, Na niwe upendanyo.

WhatsApp