21 – Baba Twakujia

( Father, We Come To Thee )

1. Bwana twakujia, Uwe msaada;
Uwe kimbilio, twakusihi.
Dunia ni giza tukitengwa nawe;
Tufariji hapa, baba yetu.

Baba twakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie.

2. Salama tulinde, kati ya taabu;
Uwe raha yetu mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie;
Twakuomba sana, tupe nguvu.

3. Neema utupe, tukubali kwako;
Moyo wetulinda, safarini;
Tuongoe mbele, tupate kushinda
Na kufika ng’ambo, kule kwako.

WhatsApp