110 – Mlango Wazi

( The Gate Ajar for Me )

1. Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:
Yesu aneufungua Na hakuna kufunga.

Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu?

2. Mlango hukaa wazi watu waokolewe:
Maskini ma matajiri Wa mataifa yote.

3. Maadanu mlango wazi, Rafiki kaza mwendo;
Msalaba ukubali- Amana ya upendo.

4. Msalaba tutabeba Daima, na furaha!
‘pendo la Yesu hushinda. Unainama kwake!

WhatsApp